Jinsi ya Kununua Domain ya .COM kwa Shilingi Tsh 3,000

Amani JosephNovember 14, 20222 min read Linapokuja swala zima la biashara ni wazi kuwa huwezi kufanya biashara kikamilifu bila kuwa na tovuti, tovuti imekuwa ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mfanya biashara na wa…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
November 14, 2022
2 min read

Linapokuja swala zima la biashara ni wazi kuwa huwezi kufanya biashara kikamilifu bila kuwa na tovuti, tovuti imekuwa ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya mfanya biashara na wateja hivyo nadhani ni muhimu sana kwa kila biashara kuwa na tovuti.

Kuliona hili hivi leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia ili kuweza kuanzisha tovuti yako kwa gharama nafuu, njia hii ni nzuri sana na endapo ikichanywa na njia nyingine za kutengeneza tovuti bila kutumia gharama yoyote ambazo tayari tulisha ziangalia hapo awali.

Basi hebu tuache maneno mengi na twende kwenye njia hii, sasa kama kichwa cha makala kinavyosema hapa tutaenda kuangalia njia ya kupata domain yenye .com ambayo ndio itakusaidia kutengeneza tovuti kwa gharama ya Tsh 3000 pekee.

Kumbuka njia hii ni bora kama unataka kufuta njia za kutengeneza tovuti ya bure ambazo zimewahi kuonyeshwa kwenye makala zilizopita.

Bofya Hapa Domain TZS 3000

Sasa kwa kuanza unatakiwa kubofya Link hapo juu kisha utapelekwa kwenye ukurasa wa tovuti ya GoDaddy ambayo ni tovuti maarufu sana kwa usajili wa domain. Kwenye ukurasa huu unatakiwa kuchagua domain ya .COM kwa gharama za hadi dollar $0.99.

Najua utakuwa unajiuliza kwanini ni dollar 0.99 ambayo ni Tsh 2,000 na mimi nina kwambia Tsh 3,000, sasa uatakapo fika kwenye sehemu ya malipo utaona gharama zimeongezeka hadi kufikia dollar $1.17 ambayo ni takribani Tsh 2700.

Lakini sasa kama huna kadi ya benki kuweza kulipia domain hii unaweza kulipia kwa kutumia Mpesa, unacho takiwa ni kufuata maelezo ya jinsi ya kutengeneza Mpesa Visa Card na baada ya kumaliza weka namba za kadi utakazo kuwa umetumiwa kwa njia ya SMS bila kusahau mwezi na mwaka wa kadi yako kuisha pamoja na CVC.

Baada ya hapo lipia na moja kwa moja utakuwa umemaliza na utapata domain yako kwa kiasi cha Tsh 3,000 tu. Kumbuka unaweza kufuata hatua hapo chini ili kuweza kuunganisha website yako pamoja na domain yako.

Pia baada ya kusajili domain yako unaweza kupata Free Hosting kwa mwaka mzima bure kabisa kwa kufuata hatua kwa hatua Hapa.

Na hiyo ndio njia rahisi sana ya kupata domain ya .COM kwa Tsh 3,000. Kama kuna mahali umekwama usiache kutuambia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tuta kusaidia moja kwa moja.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Weka Password Kwenye File Bila kutumia Programu
November 13, 2022
2 min read
Next Post

10+ Best Places to Visit in Tanzania

November 15, 2022
10 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Fanya Mambo Mengi Zaidi Kupitia Telegram Bots Hizi
November 20, 2022
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)
November 17, 2022
3 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuandika Haraka kwa Kutumia (AI) Artificial intelligence
November 16, 2022
2 min read

Related guides

Related gadgets