Facebook Kuongeza Sehemu Mpya ya Kutafuta na Kuomba Kazi
Wote tunajua ugumu ulipo katika swala zima la kutafuta ajira, ndio mana Facebook kupitia mtandao wake wa facebook sasa inakuja na sehemu mpya ya kukuruhusu wewe kutafuta mfanya kazi au kuomba kazi. Sehemu hiyo mpya itasa…
Wote tunajua ugumu ulipo katika swala zima la kutafuta ajira, ndio mana Facebook kupitia mtandao wake wa facebook sasa inakuja na sehemu mpya ya kukuruhusu wewe kutafuta mfanya kazi au kuomba kazi.
Sehemu hiyo mpya itasaidia wale wenye page za kibiashara za facebook (Business Pages) kutuma list ya nafasi za kazi kwenye kurasa zao hizo huku wale wanao penda (like) page hiyo wakipata uwezo wa kupenda (kulike), kutoa maoni (kucomment) pamoja na kuomba (kuapply) kazi moja kwa moja kwenye kurasa hizo bila kutoka nje ya mtandao wa facebook.
Kwa sasa sehemu hiyo mpya inategemewa kutoka leo kwenye nchi za US pamoja na Canada, kwa tanzania bado haijatangazwa sehemu hii inakuja lini ila ni vizuri kukumbuka kuwa sehemu hiyo itakuja kwa wale wenye kurasa za kibiashara pekee hivyo kabla sehemu hiyo haijaja Tanzania hakikisha page yako ni ya kibiashara ili uweze kupokea sehemu hiyo.
