Google Meet Njia Mpya ya Kufanya Mikutano Kwa Video

Wakati dunia ikizidi kupambana na Virusi vya Corona (COVID-19), teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video inazidi kukuwa kwa kasi sana kiasi kwamba kampuni nyingi za teknolojia sasa zinakuja na teknolojia hizo ili kuwe…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read

Wakati dunia ikizidi kupambana na Virusi vya Corona (COVID-19), teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video inazidi kukuwa kwa kasi sana kiasi kwamba kampuni nyingi za teknolojia sasa zinakuja na teknolojia hizo ili kuwezesha watu kuwasiliana kwa urahisi hasa kipindi hichi ambacho watu wanashauriwa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi.

Google ni moja ya kampuni ambazo hivi karibuni zilitangaza kuja achia njia mpya ya kuwasiliana kwa njia ya video kupitia programu yake ya Google Meet. Kama ulikuwa hujui, Google Meet hii ni sehemu ambayo ilikuwa ya kulipia kwa watumiaji wa Google Business, lakini sasa imeletwa kwa watumiaji wote bure kabisa. Kupitia Google meet mtu yoyote ataweza kuwasiliana kwa njia ya video na watu 50 kwa wakati mmoja kwa pamoja.

https://youtu.be/wkP_8vwhPtM

Kupitia Google Meet utaweza kutengeneza mkutano kwa urahisi kwa kutumia app ya Android au iOS, au kama hutaki kutumia programu hizo unaweza kutengeneza mkutano kwa urahisi kwa kutembelea tovuti ya meet.google.com. Sio lazima kuwa na app au sio lazima watu unaotaka kuchat nao kwa njia ya video wawe na programu hiyo, bali kitu cha muhimu wanatakiwa kuwa na internet pamoja na link ya mkutano ambayo utakuwa umeipata mara baada ya kutengeneza mkutano kupitia app au tovuti ya Google Meet.

The app was not found in the store. :-(

Pia kama unatumia app ya Gmail unaweza kuapa sehemu ya Meet moja kwa moja kupitia Email yako na hapo utaweza kutengeneza mikutano kwa urahisi na haraka.

Hivi karibuni njia ya video imekuwa ikitumika sana kufanya mikutano kwa watu mbalimbali, hii ni baada ya marufuku ya kukusanyika iliyokuja baada ya kuanza kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona ambayo yalianza kuripotiwa tokea mwishoni mwa mwaka jana 2019.

Mbali na Google Meet, Facebook nayo imepanga kuja na sehemu mpya ya Rooms, sehemu ambayo itasaidia watu kufanya mikutano kwa njia ya video. Sehemu hiyo mpya ya Rooms itakuwa inapatikana kwenye mitandao yake yote ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Messenger. Ambapo pia ili kutumia sehemu hiyo huna haja ya kuwa na programu nyingine yoyote.



Related guides

Related gadgets