Instagram Sasa Kuruhusu Mtu Kuomba Kujiunga na Live Video
Hivi karibuni mtandao wa instagram ulileta mabadiliko ambayo yaliwezesha watumiaji wa mtandao huo kwenye sehemu ya Live Video kualikana na kuweza kuwa mubashara kupitia video moja. Hivi karibuni mtandao huo umeboresha se…
Hivi karibuni mtandao wa instagram ulileta mabadiliko ambayo yaliwezesha watumiaji wa mtandao huo kwenye sehemu ya Live Video kualikana na kuweza kuwa mubashara kupitia video moja.
Hivi karibuni mtandao huo umeboresha sehemu hiyo na kuleta uwezo wa mtu ambaye ni rafiki yako kuomba kujiunga na Live Video yako mara tu pale unapokuwa hewani. Mara tu unapokuwa una angalia video ya live ya mtu utaona kitufes kipya cha ‘Request‘ kilichoko chini kabisa karibia na sehemu ya Comment.
Sasa kupitia App za #Instgram utaweza kumuomba rafiki yako au mtu unae mfuata (Follow) kushiriki kwenye video za live, soma hapa kujua zaidi > https://t.co/PagxCUQZWw pic.twitter.com/t5M0yFlFn4
— VinkoWeb (@VinkoWeb) November 22, 2017
Bofya kitufe hicho kisha subiria ulio muomba aweze kukubali kisha moja kwa moja utaweza kuwa mubashara kabisa kwenye video moja na rafiki yako. Japo kuwa inawezekana watu wengi kuomba kuwa live na mtu fulani lakini maombi ya mtu mmoja tu kwa wakati ndio yanaweza kukubaliwa.
Sehemu hii inasemekan kuwa itakuwa maarufu sana sababu itasaidia watu maarufu kuweza kujiunganisha na wapenzi wao kwa njia ya video, kwa sasa tayari sehemu hii inaendelea kutoka kwenye Programu zote za Android na iOs na kama bado hujaiona ingia kwenye soko la Play Store au App store kisha angalia update za programu hiyo.
