Jinsi ya Kutuma na Kupokea File la Aina Yoyote kwa WhatsApp

Wote tunajua kuwa sasa unaweza kutuma na kupokea file za pdf, docx na mp3 kwa kutumia programu ya WhatsApp, lakini mpaka sasa bado kuna aina nyingi sana za file ambazo bado haiwezekani kutumia kwa kutumia programu hiyo n…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Wote tunajua kuwa sasa unaweza kutuma na kupokea file za pdf, docx na mp3 kwa kutumia programu ya WhatsApp, lakini mpaka sasa bado kuna aina nyingi sana za file ambazo bado haiwezekani kutumia kwa kutumia programu hiyo ndio maana leo VinkoWeb tunakuletea njia hii ya kuwezesha programu yako ya WhatsApp kutuma na kupokea file za aina yoyote ile.

Kwa kuanza ni vyema kujua njia hii ni lazima watumiaji wote (anae tuma na anae tumiwa file) wawe na programu husika na vilevile njia hii inatumia mfumo wa Android pekee, hivyo kama unatumia vifaa vya Apple vyenye mfumo wa iOS itakubidi kusubiri kidogo wakati tunafanyia utafiti swala hili. Nikiwa nimesha sema hayo basi moja kwa moja twende tukangalie hatua za kuwezesha programu yako ya Whatsapp kutuma ma-file ya aina yoyote. Hatua ya kwanza ingia kwenye browser ya simu yako na fungua ukurasa huu kisha download hapa app hii. Baada ya hapo install vizuri kwenye simu yako kisha fuata hatua zifuatazo.

Related guides

Related gadgets