Agundua Kompyuta Yenye Kujua Harufu ya Kansa na Mabomu

Raia mmoja wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazo tumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini hapa Tanzania. Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya mabomu na unaweza ku…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Raia mmoja wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazo tumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini hapa Tanzania. Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya mabomu na unaweza kutumiwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, alisema.

Vilevile kifaa hicho kilicho na ukubwa wa modem na kupewa jina Koniku Kore kinaweza kuwa ubongo wa roboti za siku za usoni. Kampuni kubwa za kiteknolojia, ikiwemo Google hadi Micrososft ziko katika harakati ya kutengeza roboti inayoweza kuwa na akili ya mwanadamu, hivyo inawezekana jamaa huyu kupata nafasi kupitia kampuni hizo.

Bwana Agabi alizindua kifaa hicho cha koniku yapata mwaka mmoja uliopita na amefanikiwa kuchangisha dola milioni moja kama ufadhili na anasema kuwa kifaa hicho kimempatia dola milioni 10 katika mikataba na kampuni za usalama.

Koniku Kore ni kifaa kilichotengezwa kwa kutumia neva na silicon ambacho kina sensa zinazoweza kutambua harufu. ”Unaweza kuzipa neva hizo maelezo ya ni nini unachotaka zifanye ambapo upande wetu tunaziambia kutoa seli zinazoweza kutambua harufu”,alisema.

Kungamano la TEDGlobal limeanza toka tarehe 27 mwezi huu huko Arusha, Tanzania na linategemewa kumalizika tarehe 30 mwezi huu. Kungamano hilo lina lengo la kushirikishana mawazo mbalimbali pamoja na utatuzi wa matatizo hayo yanayo zunguka jamii.

Chanzo : CNN

Related guides

Related gadgets