Jinsi ya Ku-edit PDF kwa Kutumia Kompyuta (Windows)

Amani JosephNovember 25, 20242 min read Kama wewe ni mfutiliaji wa tovuti ya VinkoWeb ni wazi kuwa unajua jinsi ya ku-edit PDF kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kama bado hujui jinsi ya kufanya hivyo nakushauri kusoma ma…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
November 25, 2024
2 min read

Kama wewe ni mfutiliaji wa tovuti ya VinkoWeb ni wazi kuwa unajua jinsi ya ku-edit PDF kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kama bado hujui jinsi ya kufanya hivyo nakushauri kusoma makala hiyo kwanza na uhakika itakusaidia sana.

Baada ya kujaribu njia hiyo lakini unaona kuwa njia ya kutumia kompyuta ni njia bora kwako basi endelea kwa kusoma makala hii. Kumbuka njia hii ni maalum kwa watumiaji wa kompyuta za Windows hivyo ni muhimu kuwa na kompyuta yenye mfumo wa Windows kabla ya kuendelea.

Baada ya kuhakikisha unatumia mfumo wa Windows, moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini kisha download programu hiyo na install kwenye kompyuta yako. Baada ya kuinstall moja kwa moja endelea kwa kufuata maelekezo hapo chini.

Download Programu Hapa

Baada ya kuinstall programu hiyo vizuri, moja kwa moja nenda kwenye dokmenti yoyote ya PDF unayotaka ku-edit, kisha moja kwa moja fungua dokmenti hiyo kwa kutumia programu hiyo uliyo download hapo juu.

Baada ya hapo moja kwa moja sogeza kasa au mouse yako kwenye neno lolote au picha iliyoko kwenye PDF unayotaka ku-edit. Bofya mara moja kuchagua sehemu ya neno unalotaka kuedit.

Kisha baada ya hapo bofya mara mbili kwenye mstari au sehemu ya maneno au picha unayotaka ku-edit.

Kama unavyoweza kuona, sasa utaweza kubadilisha sehemu hiyo ya maneno iliyopo kwenye pdf, na kizuri ni kuwa mwandiko ulipo hauto tofautiana na muandiko unao andika kwa muda huo.

Mbali na hayo pia utaweza ku-edit picha iliyopo kwenye PDF hii ikiwa ni pamoja na logo na kila kutu kama vile sign pamoja na kila kitu kilichopo kwenye PDF.

Utaweza kubadilisha logo kwa kuchagua logo husika kisha delete au badilisha kwa kuchagua logo nyingine kutoka kwenye kompyuta yako. Baada ya ku-edit chochote hakikisha unakumbuka kusave kwa kuchagua sehemu ya File kisha bofya Save.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Ongeza Ukubwa wa Maandishi Kwenye Apps Zote (Android)
November 21, 2024
1 min read
Next Post

Tigo Tanzania Yabadilisha Jina Sasa ni “YAS”

November 26, 2024
1 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube
December 17, 2024
2 min read
  • AI Tanzania
  • Maujanja
Tumia Aina Mbalimbali za AI Kama ChatGPT Kwa Wakati Moja
December 16, 2024
1 min read
  • Maujanja
Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App
December 15, 2024
2 min read

Related guides

Related gadgets