Download Video Instagram, Twitter, TikTok, na Mitandao Mingine

Amani JosephAugust 26, 20242 min read Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapendelea kuhifadhi baadhi ya video zako kwenye kifaa chako au sehemu nyingine tofauti na kwenye mitandao ya kijamii njia hii itakuwa bora sana kw…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
August 26, 2024
2 min read

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapendelea kuhifadhi baadhi ya video zako kwenye kifaa chako au sehemu nyingine tofauti na kwenye mitandao ya kijamii njia hii itakuwa bora sana kwako.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ya kupakua video kutoka kwenye mitandao ya kijamii kwa urahisi kwa kutumia simu yako ya Android. Huna haja ya kuwa na apps nyingi kwenye simu yako kwani njia hii itakusaidia kupakua video, picha na kila kitu kwenye simu yako ya Android.

Kwa kuanza ni vyema ufahamu kuwa njia hii ni kwa ajili ya watumiaji wa simu za Android kama unatumia iOS unaweza kusoma makala yetu hapa.

Kwa kuanza unatakiwa kupakua App hapo chini, app hii haipatikani kwenye soko la Play Store hivyo ni muhimu kupakua kupitia link hapo chini.

DOWNLOAD HAPA

Baada ya kupakua app hii, Install kwenye simu yako kama APK, kisha moja kwa moja unaweza kuanza kupakua picha na video yoyote kwa urahisi na haraka sana.

TABLE OF CONTENTS

  • 1. Download Video Zako za Instagram
  • 2. Download Video Zako za TikTok
  • 3. Download Video Zako za X (Twitter)
  • 4. Mitandao Mingine ya Kijamii

Download Video Zako za Instagram

Kama unataka kupakua video yako kutoka akaunti yako Instagram unachotakiwa kufanya ni kunakili au kucopy link ya picha au video na kisha fungua app hii na inaweza kugundua link uliyonakili na kuanza kudownload moja kwa moja baada ya wewe kubofya Download.

Download Video Zako za TikTok

Pia kama unataka kupakua au kudownload video zako za TikTok hatua hazina tofauti sana na hatua za kupakua kutoka Instagram. Unacho takiwa kufanya ni kubofya sehemu ya share kwenye video yako, kisha moja kwa moja bofya copy na baada ya kunakili link moja kwa moja fungua app hii na utaweza kupakua video bila alama ya Tiktok.

Download Video Zako za X (Twitter)

Kama unataka kupakua video zako za Twitter au X, hatua inaweza kuwa tofauti kidogo lakini sio hatua nyingi kama unavyo dhani, unatakiwa kubofya kitufe cha share kwenye picha au video yako kwenye mtandao wa X, kisha moja kwa moja copy link ya tweet na fungua app hii.

App hii itakupeleka kwenye browser ya ndani ya app na tweet uliyo nakili itaonekana ndani ya browser hiyo pamoja na sehemu ya kudownload bofya kwenye sehemu hiyo kupakua.

Mitandao Mingine ya Kijamii

Kupitia app hii utaweza kupakua video zako kupitia mitandao karibia yote ya kijamii. Muhimu ni kufuata hatua kama hizo hapo juu na utaweza kupakua video zako kwa urahisi kabisa kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii.

Kama kwa namna yoyote umekwama na unashindwa kupakua video zako kutoka kwenye mtandao wowote wa kijamii basi unaweza kutujulisha kupitia sehemu ya maoni hapo chini na tuna ahidi kukupa msaada moja kwa moja.

Kama unataka kuendelea kusoma makala zaidi kwa kiswahili unaweza kupakua app ya VinkoWeb kupitia Play Store.

Price: Free

Kisha baada ya kufungua bofya Menu upande wa kulia kisha chagua Swahili Site bofya Choose na kisha chagua Kiswahili na malizia kwa kubofya Save. Kisha funga na fungua app na utakuwa unasoma habari za teknolojia kwa kiswahili kila siku.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Simu Gani Bora Upande wa Kamera.? Camon 30 vs Galaxy S24
August 23, 2024
1 min read
Next Post

WhatsApp Yaja na Username Badala ya Namba ya Simu

August 26, 2024
2 min read
You May Be Interested
  • AI Tanzania
  • Maujanja
Programu Bora za AI Kwaajili ya Watengenezaji wa Programu
September 24, 2024
3 min read
  • Maujanja
  • Programu
Convert Picha, Video na Mafile ya Aina Zote Kwa Haraka
September 6, 2024
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuchati Bure Hata Kama Huna Bando au Salio
August 27, 2024
1 min read

Related guides

Related gadgets