Jinsi ya Kupata Simu Iliyopotea kwa Kupiga “Mluzi”

Amani JosephOctober 17, 20222 min read Kwa kuanza ningependa uelewe kuwa njia hii ni kwa ajili ya mtu ambaye amepoteza simu kwenye mazingira ya nyumbani au mazingira ambayo anayafahamu. Kwa lugha nyingine njia hii itakus…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
October 17, 2022
2 min read

Kwa kuanza ningependa uelewe kuwa njia hii ni kwa ajili ya mtu ambaye amepoteza simu kwenye mazingira ya nyumbani au mazingira ambayo anayafahamu.

Kwa lugha nyingine njia hii itakusaidia kama umeweka simu yako mahali ambapo umesahau, kama unataka kujua jinsi ya kupata simu ambayo imepotea unaweza kusoma makala hii hapa kama unatumia simu ya Android, na kama unatumia iOS unaweza kusoma hapa.

Jinsi ya Kupata Simu iliyopotea

Baada ya kusema hayo moja kwa moja unacho takiwa kufanya ni kudownload app kupitia link hapo chini. Baada ya kudownload endelea kwenye maelezo hapo chini.

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii, moja kwa moja endelea kwa kuhakikisha una ruhusu app hii kutumia Mic kwenye simu yako.

Baada ya hapo utaletewa maelezo mengine unaweza kubofya Done kwenye kila maelezo kisha moja kwa moja endelea kwa kufuata hatua hizi.

Kwenye ukurasa wa kwanza utaruhusiwa kutafuta simu yako kwa kupiga Mluzi. Swipe kwenda kulia mwisho wa kioo cha simu yako kuwasha sehemu hiyo.

Baada ya kuwasha sehemu hii unaweza kubofya sehemu ya Flashlight na Vibrate ili kuongeza uwezekano wa kupata simu yako pale inapo potea kwenye mazingira unayo yafahamu. Baada ya kuwasha sehemu hiyo unaweza kufunga app hii na kisha piga mluzi na utaona simu yako ikitoa sauti kila mara unapo pia mluzi.

Pia unaweza kutumia njia ya kupata simu yako kwa kupiga makofi. Kuwasha sehemu hii bofya sehemu iliyo chorwa makofi, kisha endelea kwa kuwasha sehemu hii kama ilivyo kwenye hatua ya awali hapo juu.

Baada ya hapo unaweza kuendelea kwa kubadilisha sauti inayo tokea wakati unapiga mluzi au wakati unapia makofi, unaweza kufanya hivyo kwa kubofya sehemu ya Configurations.

Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kupata simu yako ya Android iliyopotea kwa kupiga mluzi. Kumbuka kuwa njia hii ni muhimu kwa mtu ambaye amepoteza simu kwenye mazingira ambayo anayafahamu.

  • maujanja ya android
Updated:
Previous Post
Apps (7) za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Android TV (2022)
October 13, 2022
4 min read
Next Post

New MediaTek Dimensity 9200 Coming Next Month

October 18, 2022
1 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Tafsiri Meseji ya WhatsApp kwa Lugha Yoyote
October 26, 2022
1 min read
  • Maujanja
  • Mtandao
Tovuti za Kujifunza Kutengeneza Apps na Website Bure 100%
October 24, 2022
2 min read
  • Maujanja
Tumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta
October 18, 2022
2 min read

Related guides