Hizi Hapa Apps ambazo ni Mbadala wa Soko la Play Store

Amani JosephMarch 22, 20222 min read Ukweli ni kwamba kuna watu wengi sana wanaotumia simu za Android ambazo hazina uwezo wa kupakua programu kutoka soko la play store. Hii inafanya watu wengi kushindwa kupakua kwa harak…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
March 22, 2022
2 min read

Ukweli ni kwamba kuna watu wengi sana wanaotumia simu za Android ambazo hazina uwezo wa kupakua programu kutoka soko la play store. Hii inafanya watu wengi kushindwa kupakua kwa haraka programu za muhimu au kukosa update za programu hizo kwa wakati.

Kuliona hili leo nimekuletea list ya masoko ya apps ambayo yatakusaidia kupakua apps za Android kwa urahisi, ikiwa pamoja na kupata update za apps mbalimbali kwa urahisi na haraka.

Kumbuka kuwa, Google hairuhusu mbunifu yoyote kuweka apps ambazo uruhusu watu kupakua apps nyingine ndani yake hivyo, app zote ambazo zipo kwenye list hii hazipatikani kwenye soko la Play Store na badala yake utaweza kupakua kupitia link maalum hapo chini.

TABLE OF CONTENTS

  • 1. Aurora Store
  • 2. Appvn
  • 3. Aptoide
  • 4. AC Market

Aurora Store

Aurora Store ni moja kati ya app ambayo inakupa uwezo wa kupakua app mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii inatumia mfumo kama wa Google hivyo kuna wakati unahitaji akaunti ili kuweza kupakua baadhi ya App. Lakini kifupo app hii ni nzuri sana na naweza kusema huu ni mbadala mzuri sana wa app ya Play Store kwa wale ambao simu zao hazina app hiyo.

Download App Hapa

Appvn

Appvn ni app nyingine ambayo itakusaidia kupakua app nyingi kwa urahisi na haraka, tofauti ya app hii na nyingine ni kuwa kupitia soko la Appvn utaweza kupakua app ambazo zinauzwa kwenye soko la Play Store lakini hapa utazipata bure kabisa. Unaweza kujaribu soko hili kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Aptoide

Aptoide ni app nyingine ambayo itakusaidia kupata app mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii ni kama app ya kwanza kwenye list hii na utaweza kupakua app zote ambazo zipo kwenye soko la Play Store na utaweza kupakua kwa app zote kwa kutumia app hii.

Download App Hapa

AC Market

AC Market ni app nyingine ambayo itakusaidia kupakua app nyingine kwa urahis na haraka. App hii pia ni kama soko la Play Store na app zote ambazo ziko kwenye soko la Play Store utaweza kuzipata hapa kwenye soko la AC Market. Unaweza kujaribu soko hili kwa kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Na hiyo ndio list ya apps ambazo ni mbadala wa soko la Play Store, Kama unataka kujua app nyingine nzuri zaidi ambazo zinaweza kukusaidia kupakua audio na video kwa urahisi na haraka unaweza kusoma hapa, utaweza kupata nyimbo zote mpya kwa urahisi na haraka.

Updated:
Previous Post
Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha
March 22, 2022
2 min read
Next Post

Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Picha Bila App Yoyote

March 23, 2022
1 min read
You May Be Interested
Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App
March 25, 2022
2 min read
Umuhimu wa Kurestart Simu Yako Angalau Mara 1 kwa Wiki
March 24, 2022
3 min read
Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Picha Bila App Yoyote
March 23, 2022
1 min read

Related guides

Related gadgets