Maujanja ya Kufanya Kwenye Picha Zako (Android)

Amani JosephNovember 8, 20222 min read Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupendelea kuedit picha kwa namna mbalimbali basi ni wazi kuwa lazima umeshajaribu njia mbalimbali kupitia VinkoWeb. Mbali ya njia hizo bado zipo nj…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
November 8, 2022
2 min read

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupendelea kuedit picha kwa namna mbalimbali basi ni wazi kuwa lazima umeshajaribu njia mbalimbali kupitia VinkoWeb.

Mbali ya njia hizo bado zipo njia mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kubadilisha picha zako zikawa kwenye muundo wa namna ya kipekee. Kupitia makala hii leo VinkoWeb tumekuletea njia mpya ambazo zinaweza kusaidia kuedit picha zako kwa urahisi na kisasa kabisa.

Najua uko na majukumu mengi hivyo sitapoteza muda wako zaidi na kwa kusema hayo moja kwa moja twende kwenye makala hii.

TABLE OF CONTENTS

  • 1. Badilisha Sura yako Kuwa Katuni
  • 2. Weka Rangi Kwenye Picha za Zamani
  • 3. Ondoa Background Kwenye Picha Fasta!

Badilisha Sura yako Kuwa Katuni

Kupitia hapa VinkoWeb, tumesha ongelea app nyingi sana ambazo zinakusaidia kubadilisha picha kuwa katuni, lakini pamoja na hayo bado zipo app nyingi ambazo unaweza kuzitumia kubadilisha picha zako kuwa katuni.

Kupitia app hii utaweza kubadilisha picha yenye sura yako kuwa katuni kwa asilimia 100, tofauti na app nyingine ambazo hujaribu kubadilisha picha kuwa katuni app hii huweza kufanya hatua hizi kwa asilimia kubwa kuliko app nyingi ambazo umeshwahi kujaribu. Kitu cha msingi jaribu app hii kisha utaniambia… trust me utafurahia sana matokeo.

Download App Hapa

Weka Rangi Kwenye Picha za Zamani

Ni wazi kuwa tunajua kuwa picha za zamani zilikuwa hazi rangi, ndio maana kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuweka rangi kwenye picha za zamani bila kupoteza muda mrefu.

Kama unavyoweza kuona njia hii ni bora na rahisi sana kwa mtu yeyote ambaye ni muhenga na anazo picha za zamani ambazo kwa namna moja ama nyingine hazina rangi na ungependa kuweka rangi kwa kutumia mfumo wa AI basi jaribu app hii kisha utaniambia, trust me utashangazwa na matokeo.

Download App Hapa

Ondoa Background Kwenye Picha Fasta!

Kama unataka kuondoa background kwenye picha kuna njia nyingi hapa VinkoWeb, lakini hadi sasa hakuna njia ya haraka kama hii, kupitia njia hii unachotakiwa kufanya ni kupicha picha na moja kwa moja itaondolewa background na utaweza kuiweka kwenye background nyingine moja kwa moja.

Kama unavyoweza kuona hapo juu, njia hii ni haraka na pia zipo background nyingi mbalimbali ambazo zipo ndani ya app ambazo unaweza kuzitumia kuweka picha yako. Kitu cha muhimu hakikisha unapo piga picha nyuma yako kusiwe na rangi nyingi sana ili kupata matokeo mazuri zaidi, jaribu njia hii kupitia simu yako ya Android kwa kupakua app hapo chini.

Download App Hapa

  • maujanja ya android
Updated:
Previous Post
Jinsi ya Kupata FREE Hosting Mwaka Mzima (Bure 100%)
November 8, 2022
2 min read
Next Post

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

November 9, 2022
4 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Weka Password Kwenye File Bila kutumia Programu
November 13, 2022
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuongeza Uwezo wa RAM kwenye Windows PC
November 12, 2022
3 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima
November 9, 2022
4 min read

Related guides