Jinsi ya Kutuma Meseji Zinazojifuta Kupitia Facebook Messenger

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook basi habari njema kwako, leo tutaenda kuangalia njia ya kuweza kutuma meseji zinazojifuta baada ya muda fulani kupitia app ya Facebook Messenger. Njia hii ni rahisi na inaweza…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Facebook basi habari njema kwako, leo tutaenda kuangalia njia ya kuweza kutuma meseji zinazojifuta baada ya muda fulani kupitia app ya Facebook Messenger.

Njia hii ni rahisi na inaweza kufanya kazi kama unatumia app ya Facebook Messenger, kitu cha muhimu hakikisha una update app hiyo kupitia soko lako husika Play Store au App Store, kitu kingine cha muhimu akikisha unatumia app ya Messenger na sio Messenger Lite.

Kwa kuanza ingia kwenye jina la mtu ambaye unataka kuchat naye kwenye app ya Facebook Messenger, kisha baada ya hapo bofya sehemu iliyo andikwa ‘Go to Secret Conversation.’

Baada ya hapo ukurasa mpya utafunguka wenye sehemu ya kuchat, sasa endelea kwa kuandika meseji kwenye sehemu hiyo ya kuchat kisha bofya kitufe cha saa kilichopo upande wa kushoto pembeni ya kibox cha kuchat.

Baada ya hapo endelea kwa kuchagua muda ambao ungependa meseji iweze kupote, baada ya kuseti muda kila meseji uliyo andika itakaa kwa muda ulio uchagua na itajifuta yenyewe.

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, utaweza kuruhusu meseji kudumu kuanzia sekunde tano na kuendelea, meseji zote zilizofutwa zitakuwa na alama nyeusi hivyo hazitoweza kusomeka kwa mtu yoyote.

Related guides

Related gadgets