Mozilla Yaleta Njia Mpya ya Kutuma na Kupokea Mafaili

Kuna wakati unataka kutuma faili la aina flani hivyo inakubidi kutumia njia mbalimbali kama vile email, whatsApp pamoja na programu nyingine kama hizo lakini kampuni ya mozilla ina-kuleta njia mpya ya kutuma na kupokea m…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kuna wakati unataka kutuma faili la aina flani hivyo inakubidi kutumia njia mbalimbali kama vile email, whatsApp pamoja na programu nyingine kama hizo lakini kampuni ya mozilla ina-kuleta njia mpya ya kutuma na kupokea ma-faili ya aina mbalimbali kwa urahisi kabisa.

Sehemu hiyo ambayo ipo kwenye majaribio inakupa uwezo wa kutuma ma-faili yenye ukubwa wa hadi GB 1 tu, utofauti wa sehemu hiyo ni kuwa utapewa nafasi ya kutuma ma-faili ambayo baadae yata futika ndani ya masaa 24, hivyo kila link inauwezo wa kudumu masaa 24 pekee.

Kuwezesha sehemu hiyo huna haja ya kuwa na kisakuzi cha Mozilla bali unachotakiwa kufanya ni kubofya link hapo chini kisha upload file lako kisha mtumie link mtu unaetaka apate file hilo kisha ataweza kudownload file hilo haraka kabisa bila kupoteza muda.

send.firefox.com

Njia hii ambayo imetengenezwa na kampuni ya mozilla ina semekana kuwa ni njia ambayo ni salama sana na mafaili yote yanayo tumwa kupitia sehemu hii yana kuwa encrypted hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi pale unapo taka kuitumia.

Chanzo : Tech Crunch

Related guides

Related gadgets