Mtanzania Abuni Fimbo ya Dijitali Kwaajili ya Walemavu wa Macho
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph nchini Tanzania, Coreen Swai amefikia hatua nzuri ya masomo yake kwa kutumia elimu aliyoipata chuoni hapo kuweza kufanya ubunifu wa fimbo ya kidijitali au “Smart Blind Stick”…
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph nchini Tanzania, Coreen Swai amefikia hatua nzuri ya masomo yake kwa kutumia elimu aliyoipata chuoni hapo kuweza kufanya ubunifu wa fimbo ya kidijitali au “Smart Blind Stick” kama alivyo ipa jina mwenyewe.
Coreen ameweza kufanya ugunduzi huo baada ya kuamua kufikiria namna ya kipekee ya kuwa saidia walemavu wa macho hasa pale wanapotaka kutembea safari za umbali mrefu.
Coreen ambae anasoma kozi ya Information Systems and Networking Engineering anatarajia ugunduzi huo utawasaidia walemavu wengi wa macho hasa kutokana na uwezo wa fimbo hiyo wa kutoa mlio maalum pale mlemavu wa macho anapo kutana na kitu mbele yake.
Ugunduzi huu ni moja kati ya gunduzi bora mbalimbali ambazo zimewahi kufanywa na watanzania hivyo nadhani ni wakati sasa serikali kupitia Costech na wizara husika kuona vipaji vya watanzania hasa kwenye ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Chanzo : DW Swahili
