Muigizaji The Rock Kuungana na Apple Kwaajili ya Filamu Mpya

Kama wewe ni mpenzi wa filamu pamoja na teknolojia kwa ujumla basi leo tuna habari hii njema kwaajili yako. Katika kutangaza bidhaa zake kampuni ya Apple imeingia mkataba na muigizaji maarufu nchini marekani maarufu kama…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kama wewe ni mpenzi wa filamu pamoja na teknolojia kwa ujumla basi leo tuna habari hii njema kwaajili yako. Katika kutangaza bidhaa zake kampuni ya Apple imeingia mkataba na muigizaji maarufu nchini marekani maarufu kama Dwayne Johnson au kwa jina la uigizaji “The Rock”.

Mkataba huo ambao ni katika kutangaza programu ya SIRI ya kampuni hiyo muigizaji huyo anategemewa kutoa filamu yake mpya ambayo itakuwa ikitangaza bidhaa hiyo kutoka kampuni ya Apple. Filamu hiyo ambayo imepewa jina la The Rock X Siri inategemewa kutoka hivi karibuni na tayari apple wamekuwekea utangulizi huu.

https://www.youtube.com/watch?v=ufBLI6bB9sg

Lakini mpaka sasa bado haijajulikana filamu hiyo itatoka lini lakini kwa mujibu wa tweet iliyotumwa kwenye ukurasa wa muigizaji huyo, filamu hiyo inategemewa kutoka tarehe za karibuni na kwa muonekano wa picha ya tangazo filamu hiyo inategemewa kuwa ya Action na vichekesho vya hapa na pale.

Chanzo : The Next Web

Related guides

Related gadgets