Naibu Mwenyekiti wa Samsung Kufungwa Miaka 12 Jela

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini wanataka naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung Lee Jae-yong kupewa kifungo cha miaka 12 jela. Bwana Lee anakabiliwa na mashtaka kufuatia wajibu wake katika sakata la ufisadi, iliyo…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Waendesha mashtaka nchini Korea Kusini wanataka naibu mwenyekiti wa kampuni ya Samsung Lee Jae-yong kupewa kifungo cha miaka 12 jela. Bwana Lee anakabiliwa na mashtaka kufuatia wajibu wake katika sakata la ufisadi, iliyosababisha rais wa zamani Park Gue-hye aondolewe madarakani. Imeripoti tovuti ya BBC.

Hata hivyo Inaripotiwa kuwa Lee alitoa pesa nyingi ili apate uungwaji mkono wa serikali kwaajili ya manufaa yake pekee, aidha inaripotiwa kuwa mwenyekiti huyo alikamatwa na amekuwa gerezani tangu mwezi Februari kufuatia sakata hilo.

Kwa sasa bado mwenyekiti huyo anakana kufanya lolote baya, lakini katika hali nyingine siku ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi yake, waendesha mashtaka wa korea kusini walimtaja kuwa mtu aliye nufaika kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa sakati hilo na kutaka ahukumiwe.

Waendesha mashtaka wanamlaumu bwana Lee na wakurugenzi wengine wanne, kwa kumhonga mshirika wa karibu wa Rais Park, Bi Choi Soon-sil mamilioni ya dola ili wapate kupendelewa

Waendesha mashtaka walidai kuwa ufisadi huo ulikuwa na lengo la kupata uungwaji mkono wa serikali kwa mabadiliko ndani ya kampuni ya Samsung, Hukumu ya Lee inatarajiwa kutolewa tarehe 27 mwezi huu wakati akiendelea kusota gerezani.

Chanzo : BBC 

Related guides

Related gadgets