Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Amani JosephNovember 22, 20252 min read Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa speed ya internet ni muhimu sana, haijalishi wewe una muda wa kusubiri, au wewe ni kama mimi na ungependa vitu vyote unavyo fungua kwa kut…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
November 22, 2025
2 min read

Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa speed ya internet ni muhimu sana, haijalishi wewe una muda wa kusubiri, au wewe ni kama mimi na ungependa vitu vyote unavyo fungua kwa kutumia smartphone yako vifunguke kwa haraka.

Kama hivi karibuni umekuwa ukifungua app ya Instagram na unaona app hiyo haifunguki au picha zinatumia muda mrefu kufunguka basi upo mahali sahihi. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia moja rahisi na ya haraka ambayo itaongeza speed ya Internet kwenye simu yako ikiwa pamoja na kukupa ruhusa ya kutumia baadhi ya tovuti na apps ambazo unaona zimekuwa ngumu kufunguka.

Kumbuka njia hii sio VPN na ni tofauti kabisa na VPN jinsi inavyofanya kazi kwa asilimia 100. Kama unataka kujua jinsi VPN inavyofanya kazi basi unaweza kusoma hapa makala yetu iliyopita, Kumbuka nchini Tanzania matumizi ya VPN ni kinyume na sheria hivyo ni vyema kuwa makini.

Kwa kuwa kichwa cha habari kwenye makala hii kinasema “jinsi ya kuongeza speed ya Internet kwenye simu yako”, basi leo sitapoteza muda mwingi kuelezea jinsi njia hii inavyofanya kazi. Kitu cha muhimu ni kufuata maelezo haya mafupi na nakuhahidi utaweza kutumia Twitter na app nyingine bila kuwa na VPN au kitu chochote kama hicho.

Kwa kuanza bofya link hapo chini kisha download app hiyo kwenye simu yako kisha install vizuri kabisa. Kumbuku app hii inapatikana kwenye Android na iOS na unaweza kupata app hiyo kwa kubofya link hapo chini, bila kuja kama unatumia Android au iOS.

Download App Hapa

Baada ya kuinstall na kufungua app hii moja kwa moja, kubali vigezo na masharti ya utumiaji wa app hii, kisha bofya kitufe cha Switch kilichopo katikati, bofya hapo kuwasha app hii.

Baada ya kukubali vigezo vyote ikiwa pamoja na kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja utaona alama ya 1 juu ya sehemu ya notification kwenye simu yako. Hiyo ni ishara ya kuwa umemaliza kufanya setup ya app hii na sasa uko tayari kutumia internet kwa speed.

Sasa jaribu kufungua app ya Instagram au app yoyote ambayo ilikuwa slow kama vile Twitter au app nyingine yoyote kwenye simu yako…

Bila shaka umeona kuna mabadiliko, kama kuna tatizo lolote unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutakujulisha njia bora za kutumia app hii. Kumbuka kuwa huwezi kutumia app hii sambamba na VPN hivyo ni lazima kuchagua moja.

Pia kumbuka app hii haifanyi kazi kama VPN bali hii ina angalia zaidi upande wa DNS server na kutokana na kuwa sitaki kukuchosha kwa maneno mengi basi hii itakuwa mada ya siku nyingine.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Samsung Galaxy A07 na Galaxy A17 Simu janja, Maridadi na Zenye Nguvu
November 21, 2025
3 min read
Next Post

Usinunue (Smartphone) Simu Ambazo Hazina Sifa Hizi

November 25, 2025
4 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kuzima USB Port Kwenye Kompyuta Mtu Asitumie
February 11, 2026
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone
December 5, 2025
2 min read
  • Kompyuta
  • Maujanja
Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui
December 4, 2025
3 min read

Related guides

Related gadgets