Tengeneza Muziki kwa Kutumia (AI) Artificial Intelligence

Amani JosephOctober 27, 20222 min read Ni wazi kuwa teknolojia ya (AI) au Artificial Intelligence ndio teknolojia ambayo inatarajiwa kuendelea kutumika kwa kiwango kikubwa sana kwa miaka ya karibuni. Hii ni kutokana na k…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20263 min read
Amani Joseph
October 27, 2022
2 min read

Ni wazi kuwa teknolojia ya (AI) au Artificial Intelligence ndio teknolojia ambayo inatarajiwa kuendelea kutumika kwa kiwango kikubwa sana kwa miaka ya karibuni.

Hii ni kutokana na kuwa vitu vingi unavyovitumia sasa vinatengenezwa au vinatumia mfumo wa (AI) au Artificial Intelligence ili kufanya kazi kwa usahihi. Kuliona hili kupitia hapa VinkoWeb tutaendelea kukuletea njia mbalimbali za kutumia (AI) au Artificial Intelligence.

Mara baada ya kuonyesha njia ya kuandika kwa haraka kwa kutumia mfumo wa (AI) au Artificial Intelligence, siku ya leo tumekuletea njia mpya ya kutengeneza muziki kwa kutumia teknolojia hiyo.

Basi bila kupoteza muda twende kwanza niku onyeshe jinsi ambayo mimi nimefanikiwa kutengeneza (mashup) au muungano wa nyimbo mbili kati ya nyimbo mpya ya “kufuli ya Nandy” na nyimbo mpya ya “Bia Tamu ya Marioo” na kutengeneza muziki wa Kufuli Tamu ???? yote kwa kutumia AI.

Basi kama wewe unataka kutengeneza nyimbo kama hiyo au muziki kwa ujumla basi moja kwa moja endelea kwa kusoma hapo chini.

Kwa kuanza moja kwa moja tembelea tovuti hapo chini, unaweza kutumia smartphone au unaweza kutumia kompyuta.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kutembelea tovuti hii, moja kwa moja bofya kitufe cha create kilichopo kati kati ya tovuti hii.

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuchagua ni kitu gani ambacho unataka kufanya, kwa sasa unaweza kutengeneza Mashup ambayo unaweza kuchanganya nyimbo mbili tofauti, au pia unaweza kutengeneza Mixtape ambayo unaweza kuchanganya nyimbo nyingi tofauti.

Kama unataka kutengeneza video kama ambayo nimetengeneza mimi hapo juu, unaweza kuchagua sehemu ya Mashup.

Kisha baada ya hapo moja kwa moja ingia kwenye mtandao wa YouTube na tafuta video unazotaka kuchanganya copy link ya kwanza kisha paste sehemu ya Add YouTube songs or paste a link.

Baada ya hapo bofya sehemu ya Create Mashup kisha subiri baada ya muda mfupi utaweza kuona video yako ambayo itakuwa imesha changanywa moja kwa moja na itakuwa kama nyimbo moja. Pia unaweza kutengeneza audio pekee kwa kuchanganya audio mbili kutoka mtandao wa Spotify.

Sasa unaweza kujiuliza vip unaweza kuweka nyimbo hizi kwenye YouTube..? Kwa sasa bado haikubaliki kuweka nyimbo hizi kwenye mtandao wa YouTube kutokana na Copyright.

Lakini kuna wakati mwingine unaweza kuruhusiwa kuweka nyimbo hizi kwenye mtandao wa YouTube bila kuwasha Monetization kwenye video husika.

Pia kupitia channel yetu hakikisha una subscribe kwani tunamalizia Studio zetu tayar kuanza kukuletea video zenye ubora kuhusu teknojoia na mambo mengine mbalimmbali.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Njia Bora ya Kuondoa Background kwenye Picha (Android)
October 27, 2022
2 min read
Next Post

Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android

October 29, 2022
3 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Kudownload Video Kutoka Mtandao Wowote
November 3, 2022
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuzuia SMS Sumbufu Kwenye Simu Yako
November 1, 2022
1 min read
  • Maujanja
Fahamu Sehemu Zote Mtu Alizopita kwa Kutumia Android
October 29, 2022
3 min read

Related guides

Related gadgets