Uber Yasimamisha Majaribio ya Magari Yanayo Jiendesha

Kampuni maarufu ya usafirishaji ya Uber hivi karibuni imekubwa na masaibu mengine baada ya kusitisha majaribio ya magari yake yanayo jiendesha, masaibu hayo yameikumba kampuni hiyo baada ya moja ya magari yake yanayo jie…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20261 min read

Kampuni maarufu ya usafirishaji ya Uber hivi karibuni imekubwa na masaibu mengine baada ya kusitisha majaribio ya magari yake yanayo jiendesha, masaibu hayo yameikumba kampuni hiyo baada ya moja ya magari yake yanayo jiendesha kupata ajali huko Arizona nchini marekani.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya Arizona roadway ambapo gari hilo lilipata ajali na kupinduka uku likiacha magari mengine mawili yakiwa yameumia kwa upande wa Ubavuni. Habari zilizotolewa na tovuti ya tech2 zinasema kuwa, kampuni hiyo imeamua kusimamisha majaribio ya magari hayo huku ikipisha mapolisi wa usalama wa barabarani kufanya uchunguzi ili kujua kilicho tokea.

Kwa bahati nzuri ajali hiyo haiku sababisha mtu yoyote kupoteza maisha lakini hii sio mara ya kwanza kwa magari yanayo jiendesha kupata ajali, mwaka 2016 mwendeshaji wa magari yanayo jiendesha ya Tesla aliuwawa baada ya gari linalo jiendesha kutoka kampuni ya Tesla Motors Inc kupata ajali kwa kugongana na Roli huko Williston, Florida nchini marekani, Vilevile kampuni ya Google nayo ilisha tokea kwenye vichwa vya habari kutokana na magari yake yanayo jiendesha kuhusushwa na Ajali mbalimbali za barabarani.

Related guides

Related gadgets