Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja
Amani JosephJune 25, 20222 min read Ni wazi kuwa mara nyingi kuna wakati unakuta simu imejaa apps nyingi ambazo hata huzitumi kwa wakati huo, lakini pia inapokuja swala la kufuta au (Uninstall) apps hizo bado pia inakuwa…
Ni wazi kuwa mara nyingi kuna wakati unakuta simu imejaa apps nyingi ambazo hata huzitumi kwa wakati huo, lakini pia inapokuja swala la kufuta au (Uninstall) apps hizo bado pia inakuwa ni mthiani sana kwani ni lazima kuondoa app moja baada ya nyingine.
Kuliona hilo leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuondoa (Unistall) app zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
Kwa kuanza unacho takiwa kufanya ni kuingia kwenye soko la Play Store, kisha bofya vitufe vitatu vya Menu vilivyoko juu upande wa kushoto, kisha bofya sehemu ya My apps and games. Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wenye masasisho (update) mapya ya app ulizo pakua, moja kwa moja bofya sehemu iliyo andikwa installed. Baada ya hapo bofya sehemu ya Storage kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.
Baada ya kubofya hapo ukurasa mpya utafunguka ukiwa na listi ya apps ambazo ume install kwenye simu yako, kupitia hapa utaweza kujua apps ambazo hazijatumika kwa muda mrefu, apps ambazo ni kubwa sana na apps ambazo Google wanakushauti uweze kuziondoa kwenye simu yako.
Melezo yote hayo unaweza kuyapata kwa kubofya kitufe cha kuchuja au (Filter) kilichopo upande wa kulia juu sehemu iliyo andikwa Alphabetical. Bofya hapo kisha chagua menu yoyote kati ya
- Recommended – Apps ambazo Google wanakushauri kuondoa (Uninstall) zitakuwa juu.
- Size – Apps zenye kuchukua nafasi kubwa kwenye simu yako zitakuwa juu.
- Data usage – App ambazo haijatumiwa kwa muda mrefu zitakuwa juu.
- Alphabetical – Hapa utaweza kuchagua kupanga apps kwa kufuatana na Alphabet.
Baada ya kuchagua Menu moja kati ya hizo, sasa chagua app unazotaka kuzifuta kwa kuweka tiki mbele ya jina la app husika. Kwa chini utaweza kuona kiasi cha MB au GB unazoweza kuongeza kwenye simu yako baada ya kufuta app hizo, bofya hapo kisha malizia kwa kubofya Free up MB sehemu itakayo tokea kwenye kichumba maalum kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo chini.
Baada ya hapo App hizo zita ondolewa moja kwa moja kutoka kwenye simu yako na utakuwa umeweza kuondoa apps nyingi kwa wakati mmoja kupitia simu yako ya Android.
