Video : Utani Kati ya Samsung na Apple Bado Unaendelea..
Ni kweli kwamba soko la simu janja (smartphone) linazidi kuwa gumu sana kadri siku zinavyokwenda, pengine hii inatokana na kuwepo kwa kampuni nyingi zinazo chipukia kama OnePlus na nyingine ambazo ukweli zinakuja kwa kas…
Ni kweli kwamba soko la simu janja (smartphone) linazidi kuwa gumu sana kadri siku zinavyokwenda, pengine hii inatokana na kuwepo kwa kampuni nyingi zinazo chipukia kama OnePlus na nyingine ambazo ukweli zinakuja kwa kasi sana. Sasa kwa upande wa makampuni haya makubwa njia pekee iliyobaki ili kuongeza mauzo ni kupitia ubunifu na utani wa jadi.
Wote tunajua utani kati ya Samsung na Apple haujaanza leo, kumekuwa na kesi, utani na ubishani mkubwa baina ya wateja na pia baina ya makampuni haya makubwa ya utengenezaji wa simu. Kama ulifanikiwa kupata habari hivi karibuni Samsung na Apple walifikia hatua ya hitimisho baada ya kesi yao iliyokuwa ikiendeshwa kwa muda wa miaka 8 kufikia hatua ya maamuzi kwa Samsung kuilipa Apple zaidi ya dollar za marekani milioni $538.
Sasa baada ya maamuzi haya kilichobakia pekee ni utani kati ya kampuni hizi mbili huku kila mmoja akijinadi kuwa bidhaa zake ni bora zaidi.. Angalia video hapa chini.
https://youtu.be/7trMPJNBV20
Kama unataka ufafanuzi kidogo kuhusu tangazo hili ni kuwa, kwenye tangazo hili mteja alikuwa anataka kujua kuhusu ubora wa speed ya kudownload kati ya Samsung Galaxy S9 na iPhone X, na kwa sababu Galaxy S9 inaspeed kubwa ya kudownload kuliko iPhone X, muuzaji wa duka la Apple anakosa la kusema na inakuwa mwisho wa Tangazo.
Sasa tukija upande wa ufafanuzi wa kiteknolojia, Kwa mujibu wa tovuti ya GSM Arena, Galaxy S9 ina kasi ya kudownload mara mbili zaidi ya iPhone X huku S9 ikiwa na kasi ya kudownload hadi MB 100 kwa sekunde, wakati iPhone X ikiwa na kasi ya kudownload hadi MB 50 kwa sekunde.
