Hatua za Jinsi ya Kuweka Link Kupitia Mtandao wa TikTok

Amani JosephJune 24, 20222 min read Tiktok ni moja ya mtandao maarufu kwa sasa, mtandao huu kwa sasa una zaidi ya watumiaji Bilioni 1 kila mwezi, takwimu hizi ni hadi kufikia mwezi January mwaka huu 2022. Kutokana na mta…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/October 6, 20262 min read
Amani Joseph
June 24, 2022
2 min read

Tiktok ni moja ya mtandao maarufu kwa sasa, mtandao huu kwa sasa una zaidi ya watumiaji Bilioni 1 kila mwezi, takwimu hizi ni hadi kufikia mwezi January mwaka huu 2022.

Kutokana na mtandao wa Tik Tok kutumiwa na watu wengi zaidi ni wazi kuwa kila mtumiaji anatakiwa kuwa kwenye mtandao huu. Kama bado huja download app ya Tiktok, basi huu ni muda sahihi wa kufanya hivyo.

Kupitia makala ya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kuweka link kwenye bio yako moja kwa moja kwenye mtandao wa Tiktok. Njia hii ni rahisi na unaweza kufanya moja kwa moja kwenye simu yako.

TABLE OF CONTENTS

  • 1. Badilisha Akaunti Kuwa ya Kibiashara
  • 2. Weka Link Kwenye Bio TikTok

Badilisha Akaunti Kuwa ya Kibiashara

Kwa kuanza unatakiwa kupakua app ya Tiktok, kisha tengeneza profile. Kumbuka hutoweza kuweka link kwenye bio yako hadi utakapo badilisha ukurasa wako kuwa ukurasa wa kibiashara.

Unaweza kubadilisha profile yako ya Tik Tok kuwa ya kibiashara kwa kufuata maelezo marahisi yafuatayo.

Baada ya kutengeneza kurasa yako moja kwa moja bofya kwenye profile yako kisha vitufe vitatu vya menu vilivyopo juu upande wa kulia.

Baada ya hapo moja kwa moja utaona Settings mbalimbali na chagua sehemu ya Manage account ambayo ni ya kwanza kabisa.

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Switch to Business Account. Baada ya hapo bofya Next kuendelea na fuata maelekezo yote ili kukamilisha hatua zote.

Weka Link Kwenye Bio TikTok

Baada ya kuchagua Category na kufanya setup ya ukurasa wako moja kwa moja hatua ya mwisho bofya Edit Profile.

Baada ya kubofya hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuweka link kwenye bio kwa kupitia sehemu ya Bio kama unavyoweza kuona hapo chini.

Baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuendelea kwa kutengeneza bio yako kupitia hapa, unaweza kutengeneza bio yenye mitandao yako ya kijamii, biashara au hata kitu chochote ambacho unataka kuonyesha watu.

Kwa kufuata hatua hizi utakuwa umeweza kuweka link kwenye akaunti yako ya TikTok, pia bila shaka utakuwa umeweza kubadilisha akaunti yako kuwa akaunti ya kibiashara.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Akaunti Zenye Followers Wengi Instagram Tanzania (2022)
June 23, 2022
1 min read
Next Post

Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja

June 25, 2022
2 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
  • Programu
Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake
July 2, 2022
2 min read
  • Maujanja
Tovuti za Kutengeneza Android App Bila Kuwa na Ujuzi
June 28, 2022
2 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuondoa (Uninstall) Apps Zaidi ya Moja kwa Wakati Mmoja
June 25, 2022
2 min read

Related guides

Related gadgets