Jinsi ya Kupata Namba za Simu za Zamani Ulizopoteza

Amani JosephMay 16, 20252 min read Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamepoteza namba za simu za watu ambao hapo zamani ulikuwa na namba zao basi njia hii itakusaidia sana. Njia hii bado inafanya kazi mwaka 2025 – 2026, k…

https://www.facebook.com/tanzaniatech/September 2, 20262 min read
Amani Joseph
May 16, 2025
2 min read

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamepoteza namba za simu za watu ambao hapo zamani ulikuwa na namba zao basi njia hii itakusaidia sana. Njia hii bado inafanya kazi mwaka 2025 – 2026, kitu cha muhimu hakikisha una switch kutoka page kwenda kwenye profile yako. Unaweza usoma hapa kujua hatua za jinsi ya kufanya hivyo upitia Facebook, maelezo mengine yapo kama yalivyo hapo chini.

Kupitia njia hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia mtandao wa Facebook kuweza kupata namba za simu za zamani ambazo umepoteza, njia hii ni rahisi sana na mtu yoyote mwenye akaunti ya facebook anaweza kufanya.

Sasa basi kwa kuanza unatakiwa kuwa umeingia kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia kivinjari (browser) yako kama vile Google Chrome au Opera Mini. Hakikisha una switch kwenye akaunti yako binafsi kama unatumia akaunti zaidi ya moja au kama una page mbalimbali.

Baada ya kumaliza hatua za kuswitch kwenda kwenye akaunti yako binafsi moja kwa moja bofya link hapo chini.

Tembelea Facebook Hapa

Baada ya kubofya link hiyo utapelekwa kwenye ukurasa wa Facebook ambao utakuwa unafanana kabisa na ukurasa kwenye picha hapo juu.

Utaweza kuona namba na majina zikiwa zimefichwa na ili kuweza kuona namba ya mtu bofya namba husika na moja kwa moja utaletewa namba kamili.

Kwa kufanya hatua hizo utaweza kupata namba za simu za watu ambao ulipotezana nao kupitia mtandao wa Facebook. Kumbuka unaweza kupata namba zote ikiwa pamoja na majina kamili jinsi ambayo ulikuwa umesave hapo awali ulipo poteza.

Kumbuka njia hii inafanya kazi kwa simu yoyote au kompyuta na unaweza kupata namba kwa urahisi na haraka bila kujali aina ya kifaa au simu unayo tumia.

  • maujanja
Updated:
Previous Post
Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta
May 16, 2025
3 min read
Next Post

How to Choose The Best Camera for Photos and Videos

May 17, 2025
5 min read
You May Be Interested
  • Maujanja
Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone
December 5, 2025
2 min read
  • Kompyuta
  • Maujanja
Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui
December 4, 2025
3 min read
  • Maujanja
Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako
November 22, 2025
2 min read

Related guides

Related gadgets